Ukaribu wake kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa
ulikukutanisha na stori za Diamond Platnumz kuwa amekua na uhusiano wa kimapenzi
na mwanamitindo wa bongo Hamisa Mobetto.
Stori zilianzia kwenye birthday party ya mama Diamond baada ya Hamisa
kuonekana kuwa karibu na familia hiyo hasa dada wa Diamond lakini pia
kuna picha iliyosambaa inaonyesha wawili hao kila mmoja amepiga picha
kwa wakati wake lakini kwenye mazingira ya chumba yanayofanana
.
Diamond Platnumz ametolea
ufafanuzi ishu hiyo na kusema “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana
kwasababu yupo katika industry hizi za kufanya fashion, nimekua nikimjua
muda mrefu kidogo na sikuwahi kuwa na matatizo nae yoyote sababu
tumekuwa ni watu tu ambao tunaheshimiana …..”
"Sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikua kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na nafikiri hiyo imechangia kuingiza hayo maneno, kufanya video Tanzania mara nyingi huwa inaleta manenomaneno"

Sikiliza hapa chini:
Post a Comment