Chokochoko za Nduli Iddi Amin
Dada, kuichokoza Tanzania hadi kupelekea kuanza kwa vita iliyomfaya
aikimbie nchi yake mwaka 1978, ulikuwa ni Mto huu wa Kagera, ambapo
alikuwa akitaka mto huu ndiyo uwe mpaka halisi unaotenganisha nchi yake
ya Uganda na Tanzania. Jambo hilo lilimkasilisha sana Baba wa taifa
Mwalimu Julius Nyerere, aliyeamua kumuadabisha baada ya yeye kutangaza
kwa kejeli kubwa kuwa anauwezo wa kuisambaratisha Tanzania, na kwamba
alikuwa na uwezo wa kuwa anapata chakula cha mchana Jijini Dar es Salaam
huku akiendelea kushambulia.

Baada ya Idd Amin kuona Majeshi
ya Tanzania tayari yameshajiandaa kwa vita na yakizidi kusonga mbele
kuelekea nchini kwake, aliamua kuvunja Daraja la mto Kagera kwa bomu,
pamoja na Kanisa hili la Kyaka, lililopo pembezoni kabisa mwa Mto huo,
ambalo kwa sasa limebaki kuwa sehemu ya kumbukumbu ya Vita hiyo
iliyosababisha vifo vya askari wetu Mashujaa kadhaa, ambao hukumbukwa
kila Julai 25, kila mwaka.
Sehemu ya Makaburi ya Mashujaa
wa Tanzania, waliokuwa mstari wa mbele kuitetea Tanzania, kuhakikisha
wanamuondoa Nduli Idd Amini, hapa wakiwa wamelazwa katika makaburi
yaliyopo Kambi ya Kaboya Mkoani Kagera.
Mnara wa Mashujaa, wenye majina ya Askari wetu Mashujaa waliojitolea kuitetea Tanzania.
Hii ni sehemu ya maonyesho iliyobaki kuwa kumbukumbu ya Vita hiyo kwa vizazi na vizazi.
Hii ni Injini ya Ndege ya Jeshi
la Nduli Iddi Amini aliyekuwa Rais wa Uganda, iliyolipuliwa kabla ya
kushambulia Kanisa la Kyaka mwaka 1978.
Hii ni Gari aina ya Jeep iliyokuwa ikitumiwa na Majeshi ya Nduli Iddi Amini wa Uganda, iliyokuwa ikitumika kufanya Doria.
Hii ni mabaki ya gari aina ya Unimog iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika vita hiyo ya mwaka 1978.
Hii ni gari aina ya Jeep, pia ilikuwa ikitumiwa na Jeshi la Nduli Iddi Amini.
Hii ni Gari aina ya Benzi, lililokuwa likitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakati wa Vita hiyo.
Hii ni gari aina ya Unimog iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Vita ya mwaka 1979.
Hii ni Rada ya Kirusi iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wakati wa Vita hiyo kuanzia mwaka 1978-79.
Hili ni moja kati ya Madaraja
yaliyokuwa yakitumika kuvusha Askari baada ya Daraja la Mto Kagera la
Kyaka kulipuliwa na Jeshi la Uganda.
Hili ni Bomu la Ndege ya Jeshi la Nduli Iddi Amini, lililolipuliwa na Majeshi ya Tanzania.
Post a Comment