Kala Jeremiah asimulia jinsi Video ya wimbo wake mpya ‘Wana Ndoto’ ilivyomtoa jasho
Haikuwa rahisi kwa Kala Jeremiah kuikamilisha ngoma yake mpya, Wana
Ndoto. Ni kwasababu wimbo huo aliurekodi mwanzo mwaka 2013 lakini
producer aliyeutayarisha alishindwa kumkadhi.
Baada ya kumpiga chenga kwa muda mrefu, rapper huyo alikata tamaa
hadi mwaka 2016 alipopata mtoto, Alama. Amesema mtoto wake huyo alimpa
tena hamu ya kuufanya tena wimbo huo lakini tatizo ni kuwa daftari
lililokuwa na mashairi hakujua lilipo.Alilitafuta kwa zaidi kwa wiki mbili bila mafanikio lakini alikuja kulipata wakati akitafuta kitu kingine kabisa. Hata hivyo kazi nyingine ikaja kumpata Mtoto Miriam Chirwa aliyeimba chorus ya wimbo huu kwasababu alikuwa shule nje ya Dar.
Ilimbidi amsubiri hadi afunge shule ndipo wakaingia studio kurekodi. Msikilize Kala akisimulia zaidi kwenye interview hii.
Post a Comment