Panapokuja suala la kuonesha fedha, saa za bei ghali na cheni za madini ya thamani, hakuna anayeweza kuwafikia Diamond na Jux.

Staa wa ‘Looking For You’ na boyfriend wa Vanessa Mdee amekohoa huko Instagram na kuwaacha mashabiki wake wakiwa na maoni tofauti.
Kwenye picha ya kwanza aliyopost, kunaonekana saa ya kifahari, cheni za dhahabu na miwani za bei huku akiishia kuwatakia tu usiku mwema mashabiki.

Jux anafahamika kwa kuishi maisha ya kifahari huku fedha zake nyingi zikitokana na biashara anazofanya.
Post a Comment