Jose
Chameleon anaaminika kuwa mmoja wa wasanii wakubwa wa Afrika Mashariki
aliyeupeleke muziki wa Afrika Mashariki kimataifa. Jose ameutawala
muziki wa Uganda kwa miaka mingi hadi kufikiwa mahala pa kupewa cheo na
kuitwa Dr. Joseph Chameleon.
Hivi karibuni akifanya mahojiano na
kituo kimoja cha televisheni nchini Uganda, Jose alikuwa akizungumzia
kuhusu muziki wa Afrika Mashariki akafiki sehemu alipoulizwa kama
anaamini kuwa Diamond Platnumz kutoka Tanzania ni msanii mkubwa Afrika
Mashariki.
Akijibu swali hilo, Chameleon alisema
kuwa kuna tofauti kubwa kati ya msanii wa kwenye jukwaa na msanii wa
kwenye mitandao na Tv. Alisema Diamond Platnumz sio msanii mkubwa kama
wengi wanavyofikiri licha ya yeye kuwa maarufu kwenye mitandao ya
kijamii kama Instagram.
Alisema hata alipokuja Uganda,
alishindwa kujaza watu kwenye moja ya Club ndogo ya burudani tofauti na
yeye akija Tanzania kiasi anaweza kujaza hata uwanja wa mpira.
Jose Chameleon hamtambui Diamond kama
msanii mkubwa kwani anaamini yeye ndiye anaeshika usukani wa muziki wa
Afrika Mashariki. Alisema Diamond ni msanii anayekuzwa na mitandao ya
kijamii na Tv.
Post a Comment