[6] [recent] [slider-top-big] [Music]
You are here: Home / Alikiba ni mkubwa kuliko Davido na Wizkid Lubumbashi,– asema staa wa filamu wa DR Congo

Alikiba ni mkubwa kuliko Davido na Wizkid Lubumbashi,– asema staa wa filamu wa DR Congo

| No comment
Alikiba ni msanii mkubwa kuliko Davido na Wizkid jijini Lubumbashi, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kwa mujibu wa staa wa filamu wa nchini humo, Iqbar Mohamed Bagati.
Mohamed2 Iqbar Mohamed Bagati
Lubumbashi ni mji wa pili kwa ukubwa DR Congo baada ya Kinshasa.
Akiongea na Bongo5, Mohamed ambaye yupo nchini alipokuja kutengeneza connection na waigizaji wa Tanzania, amedai kuwa Alikiba anaweza kujaza uwanja wa mpira hata kwa siku tatu mfululizo kwa jinsi anavyokubalika huko.http://getmziki.com/wp-content/uploads/2012/01/ally_kiba_img.jpg
Amesema kuwa staa huyo wa ‘Aje’ ni kipenzi cha watu wengi jijini humo hususan wanawake.
“Alikiba anamshinda Davido, Wizkid, labda tunaweza kumlinganisha na akina P-Square huko Lubumbashi,” amesema Mohamed. Davido alishawahi kutumbuiza mjini humo kwa takriban mara nne na P-Square karibu mara mbili.
“Alikiba ni maarufu sana Lubumbashi.”