[6] [recent] [slider-top-big] [Music]
You are here: Home / , Video: Davido na Trey Songz wakutana tena Marekani, collabo yao yakamilika

Video: Davido na Trey Songz wakutana tena Marekani, collabo yao yakamilika

| No comment

Msanii wa Nigeria, Davido amepost kipande cha video kinachomuonyesha
akiwa kwenye klabu moja ya usiku huko Atlanta akiwa na staa wa Marekani,
Trey Songz wakiashiria ule wimbo wao walioahidi kuwa upo tayari.

 

 

Kwa mara ya kwanza Davido alionana na Trey Songz nchini Nigeria,
Disemba mwaka jana staa huyo alipotembelea nchi hiyo kwa ajili ya
kufanya show kwenye tamasha la Rhythm Unplugged, lakini kwa sasa
wameonekana kukamilisha ahadi ya wimbo wao walioahidi kufanya collabo
mbele ya mashabiki wa Nigeria.

Inadaiwa kuwa jina la wimbo huo ni ‘Won Le Ba’ na umeandaliwa na
mtayarishaji wa muziki, Shizzi. Davido amekuwa kimya bila ya kutoa wimbo
wowote tangu aliposaini dili na kampuni ya Sony Music, Januari 21 mwaka
huu.

Watch Video Here