[6] [recent] [slider-top-big] [Music]
You are here: Home / Rais Magufuli aijibu kampeni ya upinzani ya kuziba midomo

Rais Magufuli aijibu kampeni ya upinzani ya kuziba midomo

| No comment


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
ameijibu kampeni iliyoanzishwa na upinzani ya kuziba midomo yao kudai
kuwa serikali ya awamu ya tano imekosa demokrasia.

Alikuwa akihutubia Alhamis hii ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi uliopita.

“Niwaombe wanasiasa wenzangu, ushindani wa sasa hivi wa vyama vya
siasa ambao unatakiwa upigiwe nguvu zaidi ni kwa wale wawakilishi
waliopewa mamlaka na wananchi. Kama ni kwa madiwani wakapeleke hoja kwa
nguvu sana kwenye maeneo yao,” alisema.

“Kama ni wabunge wakazungumze kwa nguvu zote bungeni lakini hata
kuziba midomo nayo ni demokrasia,” aliongeza na kusababisha kicheko
kwenye ukumbi wa ikulu jijini Dar.

“Kwahiyo hiyo ndio demokrasia ya muelekeo ya aina yake.”

 Hivi karibuni, wabunge wa upinzani walisusia vikao vya bunge na kuziba
midomo yao kwa makaratasi wakidai kutokuwepo kwa demokrasia.