Maafisa
5 wa polisi wa Kenya wameuawa mapema leo mjini Mandera katika
shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al
shabab kutoka Somalia.
Kamishna
wa jimbo hilo la kaskazini mashariki mwa Kenya bwana Job Borongo
ameithibitishia BBC kuwa wapiganaji hao walifanya shambulizi la kuvizia
dhidi ya msafara wa magari ya polisi uliokuwa ukienda El Wak wakitumia
guruneti.
Maafisa hao tano waliangamia papo hapo huku gari walimokuwa wakisafiria likiharibiwa kabisa.
Maafisa wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.
Msafara
huo wa polisi ulikuwa ukitoa ulinzi kwa msafara wa mabasi ya uchukuzi
wa umma, desturi iliyoanzishwa baada ya wapiganaji hao kuteka basi moja
na kuua abiria 28 wakristu.
Gavana
wa Mandera bwana Ali Roba aliwalaumu maafisa wa polisi katika eneo hilo
kwa kupuuza tahadhari iliyotolewa na wenyeji kuhusiana na mashambulio
ya kigaidi.
Roba anasema walipuuza vyanzo vya kiintelijensia vilivyotolewa kuhusiana na kuonekana kwa wapiganaji hao waliojihami.
Hii si mara ya kwanza Mandera kushuhudia mashambulizi ya al shabaab.
Shambulizi
hilo la Novemba mwaka wa 2014 liliwaacha wasafiri wengi wasiokuwa
waislamu na hofu ya kusafiri na hivyo kuilazimu serikali kutoa usalama
kwa mabasi ya uchukuzi wa umma.
Mwezi mmoja baadaye wapiganaji hao waliwaua wachimba migodi 36 katika eneo hilo la Mandera.
Kundi
hilo la wapiganaji wa kiislamu limekuwa likitekeleza mashambulizi
katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya likitaka kuishinikiza taifa hilo
jirani kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Kenya ilipeleka vikosi vyake vya jeshi nchini Somalia mwaka wa 2011 ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara.
Image captio
Hata
hivyo kundi hilo limeongeza mashambulizi nchini kenya ikiwemo mauaji ya
watu 67 katika maduka ya Westgate mjini Nairobi mwaka wa 2013.
Mwaka uliopita Al Shabab ilitekeleza mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148
MakambakoTv.com does not store any files. Everything posted is for promotional use only. Files downloaded should only be kept for 24 hours and then deleted. All music and videos are copyrights to the original owners. Please support the artists and buy their work.
Thank You For Visiting MakambakoTv.Blogspot.com
Post a Comment