Msanii wa Bongo Fleva Udeude aliyefariki dunia tarehe 4 mwezi Agost
mwaka huu amezikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam usiku
wa kuamkia tarehe 5.
Marehemu
ameacha mke na mtoto huku baadhi ya watu wake wa karibu pamoja na Bob
Junior, Bonge la Nyau na muandaaji wa muziki wa Bongo Fleva Alonem
ambaye ndiye aliyekuwa wa mwisho kufanya kazi wakiongoza mazishi.
Mungu awatie nguvu ndugu, jamaa pamoja na wadau wote wa tasnia nzima
ya muziki wa bongo fleva nchini. Mungu ailaze roho yake mahala pema
peponi Amen.

Post a Comment