
Muigizaji wa filamu ya ‘Bado Natafuta’ Gabo Zigamba amenusurika kifo
katika ajali ya gari wakati akielekea hifadhi ya Ruaha akiwa na wenzake
wawili ambao wamejeruhiwa huku yeye akisalimika katika ajali hiyo.
Gabo amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki katika ajali hiyo.
Gabo amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki katika ajali hiyo.

“Uongo unaoishi ndiyo ukweli mpaka ukanushwe, nami naanzia hapa kwenye
kukanusha, ni kweli nimepata ajali lakini sijafa na maumivu ni ya ndani
sana,” aliandika Gabo katika istagram yake. “Na sijavunjika kama watu
wanavyosema ila naumia na jinsi watu wanavyowaombea wenzio Mabaya,”

Aliongeza, “Nilikuwa na lengo zuri la kugawana umasikini na wanyonge
wenzangu na hata Mungu akanisimamia. Eee Mollah wasamehe kwani na mimi
nimewasamehe, naamini utaniongoza na kunisimamia leo, kesho na hata
milele,”

Post a Comment