
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amezindua kiwanja cha mpira wa
kikapu na netball katika shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani
kilichojengwa na mwanamitindo mjasiriamali, Jokate Mwegelo.
Bi. Mjema aliwataka wanafunzi kutumia uwanja huo kwa faida ya kukuza
michezo pamoja na elimu na kumpongeza Jokate kwa alichokifanya.
“Juu ya yote hayo uliyofanya lengo ni kutaka watoto wa kike na
wenyewe wawe na kiwanja cha mpira hongera sana kidoti, hili jambo huwa
sio rahisi sana, tuna watu wangapi wanaweza kutengeneza viwanja kama
hivi hata kumi, lakini wewe kwa kile kidogo ulichokipata ukasema hapana
mimi ujuzi wangu na experience na yale niliyopata ngoja nisaidie,”,
alisema Bi. Mjema.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo alisema, “Mimi
naamini michezo ni kitu hamasishi kwa wanafunzi kufanya vyema pia katika
masomo yao na kufaulu ni wazi kuwa moja ya changamoto kubwa nchini.
Ukosefu wa viwanja bora ambavyo hukwamisha wachezaji chipukizi kuonyesha
vipaji vyao ipasavyo,” alisema Jokate.
Alisema ataendelea kujenga viwanja katika shule mbalimbali kwa faida
ya wanafunzi. Jokate ameshiriki ujenzi wa uwanja huo akishirikiana na
taasisi ya Modern Foundation.

Post a Comment