Error 404 - Not Found
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
Siasa
Madiwani wa UKAWA Wasusia Kikao cha Paul Makonda Kwa Madai Kwamba Anawadharau
Madiwani wa UKAWA Wasusia Kikao cha Paul Makonda Kwa Madai Kwamba Anawadharau
Madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya
Kinondoni wamesusa kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kwa madai kiongozi huyo hana uhusiano mzuri na
viongozi wa upinzani. 

Jana, Makonda aliitisha kikao cha wakuu wa wilaya,
wakurugenzi, wakuu wa idara za manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni
na madiwani wote, wakiwamo wabunge wanaounda halmashauri hizo.
Kikao
hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Arnaoutoglou kililenga
kuzungumzia masuala mbalimbali, kama maeneo yaliyovamiwa na uboreshaji
wa elimu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, meya wa
Kinondoni, Boniface Jacob alisema Makonda amekuwa na tabia ya kudharau
na kutoheshimu viongozi wenzake, hasa wa upinzani akiwaona hawatendi
kazi vizuri.
Pia, Jacob alidai kuwa Makonda amekuwa na tabia ya
kuingilia kazi zinazofanywa na viongozi wengine kwa kutumia cheo cha
ukuu wa mkoa, jambo ambalo meya huyo alisema ni kinyume cha sheria.
“Akitaka tumpe ushirikiano, Makonda abadilike la sivyo mtindo utakuwa
huuhuu, mambo yatakuwa hivi. Huu ni mwanzo na ndiyo maana leo (jana)
Ukawa Kinondoni tumekuwa na msimamo mmoja,” alisema Jacob.
![]() |
Jacob Diwani Wa Ubungo (Chadema) |
Jacob, ambaye
pia ni diwani wa Ubungo (Chadema), alisema hawakuona umuhimu wa kwenda
katika kikao hicho kwa sababu kiongozi wa mkutano huo anawadharau.
Akijibu tuhuma hizo, Makonda alisema madiwani waliohudhuria kikao hicho
maeneo yao yalikuwa na shida na yanahitaji kushughulikiwa, hivyo si kazi
yake kuhesabu watu na kubaini nani hakufika mkutanoni.
Alisema ajenda
kuu ya kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana namna bora ya kuvirudisha
viwanja vilivyochukuliwa na kuvirejesha kwa matumizi yaliyokusudiwa.
“Huyo anayelalamika mwambie huo anaoufanya ni utoto akikua ataacha.
Narudia tena siyo kazi yangu kuangalia nani hajaja kwenye kikao,”
alisema.
Kwenye kikao hicho, meya wa Ilala (Chadema), Charles Kuyeko
alikuwapo kwenye mkutano huo pamoja na madiwani wenzake, sambamba na
wale wa Temeke.
Makonda si mgeni wa tuhuma .Aliteuliwa kuwa mkuu wa
wilaya ya Kionondoni katika kipindi ambacho alikuwa akituhumiwa kuhusika
kwenye sakata la kupigwa kwa Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba
kwenye mdahalo wa Katiba uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl.
Katika
kipindi hicho, Makonda pia alikuwa akituhumiwa kumrushia tuhuma za
ufisadi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiahidi kuwa CCM
isingempitisha kugombea urais.
Akitoa majumuhisho ya kikao cha jana
kilichoanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi, Makonda aliwataka
watu waliovamiwa na kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kuanza kubomoa
majengo yao kabla ya Serikali kuwafikia.
Kabla ya kutoa majumuisho hayo,
Makonda alitoa nafasi kwa madiwani wa manispaa hizo kueleza kero
zinazowakabili, hususan zinazohusu ardhi.
“Najua mchakato huu utawagusa
hadi vigogo, lakini mimi siogopi vita kwa sababu ndani yangu ninaongozwa
na Mungu pekee,” alisema Makonda.
Mbali na hilo, Makonda
alisema endapo mtendaji wa ardhi atayebainika kuhusika katika kuchezea
michoro na ramani ili aachie ardhi na kujipatia fedha, atashughulikiwa
kwa mujibu sheria.
Katika hatua nyingine, Makonda amemwagiza kamishna
msaidizi wa ardhi wa Kanda ya Dar es Salaam, Mathew Nhange kumwambia
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi awaondoe
maofisa ardhi na mipango miji wa Kinondoni na Ilala baada ya kushindwa
kutoa taarifa za kuridhisha katika mkutano huo.
Huku akiwataja maofisa
hao wanaotoka Kinondoni na Ilala, Makonda alisema alishakutana na wakuu
wa idara kwenye vikao vilivyopita, hivyo alitegemea kuwa watumishi hao
wangetoa taarifa zilizokamilika. 

“Kamishna naomba umwambie katibu mkuu
mimi siwataki watumishi hawa katika manispaa hizi. Mwambie awatoe na
kuwapangia kazi nyingine,” alisema Makonda.
Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.
Kamishna Nhange alisema agizo hilo analifanyia kazi na kwamba atampa katibu mkuu taarifa za watumishi hao jana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
DISCLAIMER
MakambakoTv.com does not store any files. Everything posted is for promotional use only. Files downloaded should only be kept for 24 hours and then deleted. All music and videos are copyrights to the original owners. Please support the artists and buy their work.
Thank You For Visiting MakambakoTv.Blogspot.com
HABARI KUU
7 Android Apps You Must Uninstall From Your Phone Immediately
Apr 28, 2017|No comment
New VIDEO: French Montana ft Swae Lee – Unforgettable
Apr 15, 2017|No comment
JOTI TV – 18 Role Call ya Bwana Shamba (Episode 18) || Watch & Download Link
Sep 03, 2016|No comment
Video : Mkubwa Fella aonyesha Nyumba Mpya 4 Za Yamoto Band
Sep 03, 2016|No comment
Safi saana bieber
Teknolojia
7 Android Apps You Must Uninstall From Your Phone Immediately
Apr 28, 2017 | No comment
With new technology being introduced every hour these days there is literally an app for everythin...UJERUMANI WAZINDUA GARI LINALOANGAZA (THE TRANSPARENT CAR )
Jul 26, 2016 | No comment
Unatumia Android?? Na Unapenda Photo Editing, Hii Inakuhusu Apps 4 Ambazo Ni Nzuri Kwa Photo Editing Zaidi Ya iOS Prisma
Jul 15, 2016 | No comment
Hummingbad: Kirusi kilichoteketeza zaidi ya Smartphone mil. 10
Jul 09, 2016 | No comment
Wanafunzi wa nchini China na Teknolojia katika Kuibia Mitihani
Jun 16, 2016 | No comment
Siasa
Madiwani wa UKAWA Wasusia Kikao cha Paul Makonda Kwa Madai Kwamba Anawadharau
Aug 04, 2016 | No comment
Madiwani wa Ukawa wa Manispaa ya Kinondoni wamesusa kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa ...Tundu Lissu Atiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi baada ya kufanya mkutano wa hadhara Akiwa Singida.....Msigwa Ahutubia Iringa, Adai Serikali Imekurupuka Kuhamia Dodoma
Aug 03, 2016 | No comment
Bilionea wa Chadema Mustapha Jaffer Sabodo Amuunga Mkono Rais Magufuli....Aahidi Kutoa Trilioni 10 za Kuwekeza Dodoma
Aug 02, 2016 | No comment
Wabunge wa Ukawa waendelea kususia vikao vya Bunge
Jun 20, 2016 | No comment
Post a Comment