Awali kulikuwa na vita nzito kati ya Wema na Gigy ambapo wakati Wema
akiendelea kupalilia penzi lake, Gigy aliibuka na kudai kuwa,
atahakikisha anampata Idris akiamini kuwa ndiye mwanaume wa ndoto zake.

Kufuatia vita hiyo ambayo iliibuka baada ya Gigy kunaswa na Idris
usiku wakiwa kimahaba kwenye ukumbi mmoja wa burudani uliopo Mikocheni
jijini Dar, Wema hakuonesha kujali badala yale aliendeleza msimamo wake
kuwa yeye ndiye ‘Mrs’ Idris na wengine waliokuwa wakijipendekeza
hawakuwa na chao.
Kufuatia Wema kukomalia penzi lake, Gigy alijishtukia na kuamua kukaa
pembeni licha ya kwamba mara kadhaa alikuwa akisema kuwa ipo siku
atatimiza ndoto yake ya kutoka na Idris. 

“Mimi kwa kweli nampenda sana Idris, najua yuko na Wema lakini ipo
siku kile ninachokiwaza kitatimia,” alisema Gigy miezi kadhaa iliyopita
akionesha kuwa hatakata tamaa kupigania penzi la mshikaji huyo.
Katika kile ambacho kilionekana ni furaha kwa Gigy, hivi karibuni
Idris aliibuka na kusema kuwa, yeye na Wema wameachana na vile
walivyoonekana pamoja kwenye ile shoo ya Black Tie iliyofanyika kwenye
Ukumbi wa King Solomoni, Upanga jijini Dar mwezi uliopita ilikuwa
‘kupritendi’ tu.
Katika kuonesha kuwa kweli amefunga ukurasa wa mapenzi na Wema, Idris
alisema kuwa, siku si nyingi atamtangaza mpenzi wake mpya, jambo ambalo
lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi.
Baada ya Idris kutoa tamko hilo, siku chache baadaye alionekana
akijiachia ‘kimalovee’ na Gigy ambapo alipoulizwa kama mwanadada huyo
aliyefungashia kinoma ndiye aliyechukua nafasi ya Wema, hakuwa tayari
kuongea lolote ila Gigy alipotafutwa alisema kuwa, sasa ni mwendo wa
mahaba niue.
Akizungumza na chanzo hicho hivi karibuni, Gigy alisema
kuwa, Wema amechemka katika suala la kumzalia Idris aliyekuwa na hamu ya
kuitwa baba, sasa yeye atahakikisha ndani ya siku chache zijazo anabeba
mimba.
“Nilisema kwamba ipo siku ndoto yangu itatimia, Mungu kaniona na sasa
najitahidi sana nisichukue siku nyingi niwe nimembebea mimba Idris na
kumzalia mtoto.
“Unajua mimi nikimpenda mtu bwana inakuwa ni shida na lazima
nimfanyie kitu ambacho kitakuwa historia, naweza kusema nina jini mahaba
ambaye ananisumbua hivyo mkiniona kitumbo ndii, mjue ndiyo vile…”
alisema Gigy.
Kufuatia kujigamba huko kwa Gigy,chanzo kimoja kilimtafuta
Idris na kumuuliza kama kweli amejiandaa kuzaa na msanii huyo ambapo
kama kawaida yake alisema ni kweli wako karibu na ukaribu wao unatokana
na kwamba wanafanya kazi pamoja katika Kituo cha Redio cha Choice FM ila
hayo mengine hataki kuyazungumzia.
Ikumbukwe kwamba, hata wakati Idris anaingia kwenye uhusiano na Wema
alikuwa mzito kukubali lakini baadaye Wema akaamua kuweka mambo
hadharani kwani mwanadada huyo si mtu wa kuwa kwenye penzi la kificho.
Post a Comment