Kirusi hichi kinasemekana kuharibu simu janja zenye kutumia programu endeshaji maarufu ya Android na iOS(kwa mara ya kwanza), kimeharibu zaidi ya simu janja milioni 10 na zaidi.
Kwa muujibu wa taarifa kutoka Check Point zinasema
kuwa kirusi hicho kina uwezo wa kuathiri simu janja au tablet na kuweza
kudukua taarifa mbalimbali muhimu kutoka kwenye barua pepe,
taarifa zako za benki na kingine chochote kitakachohitajika ili kuweza
kukamilisha uhalifu na kisha kuuza taarifa hizo kwa wezi wa mitandaoni.
Jinsi kirusi hicho kinavyoathiri simu janja/tablet zenye kutumia Android/iOS
Iwapo mtu atatembelea tovuti ambayo siyo
ya kweli, kirusi hicho kitajaribu kuingia kwenye simu janja/tablet na
kujaribu kupata ruhusa ya kufanya/kuona kila kitu (root access) na
ikishindikana kirusi hicho kitajaribu kumuwezeshesha mtu kuweza kufanya
karibu kila kitu kwenye tovuti aliyoitembelea mfano unapoambiwa ubonyeze linki fulani kuweza kuangalia video ya ngono.
Kama hayo yote mawili yakishindikana kirusi hicho kitatuma
taarifa ya uwongo kukujulisha(notification) uweze ku-update simu
janja/tablet yako na ukidanganyika na kuruhusu maboresho
kufanyika(updating) basi kirusi hicho kitakuwa kimepata ruhusa ya
kudukua taarifa zako na kuziuza kwa wezi.
Taarifa zinasema kuwa Uchina kirusi hicho kimeathiri sana vifaa ya kielekroniki(simu janja/tablet) kwa wingi zaidi, takribani vifaa 1.6m ikifuatiwa na India(1.35m), Marekani ikiwa nafasi ya tatu katika idadi ya simu janja/tablets ikifuatiwa na Australia na Uingereza kwa pamoja jumla ya vifaa 100,000 vikiharibiwa na kirusi hicho.
Chati ikionyesha nchi zilizoathiriwa na kirusi hicho chenye kuathiri simu janja/tablet |
Google wanasema kuwa wanataarifa kuhusu kirusi hicho na wamekuwa
wakizuia apps zilizokwishaharibiwa na kirusi hicho kuweza kupakuliwa na
kuboresha kompyuta zao ili kuweza kuufanya taarifa za wateja wao kuwa
salama zaidi.
Post a Comment