[6] [recent] [slider-top-big] [Music]
You are here: Home / , FULL STORY: ALI KIBA NA BARAKA DA PRINCE WASHAMBULIWA NA KUNDI LA WATU 6 WENYE BUNDUKI SOUTH AFRICA

FULL STORY: ALI KIBA NA BARAKA DA PRINCE WASHAMBULIWA NA KUNDI LA WATU 6 WENYE BUNDUKI SOUTH AFRICA

| No comment

ALI KIBA NA BARAKA DA PRINCE WASHAMBULIWA NA KUNDI LA WATU 6 WENYE BUNDUKI SOUTH AFRICA

Waimbaji maarufu kutoka Tanzanian Ali Kiba na Barakah Da Prince wameshambuliwa na kundi la watu 6 wenye silaha jana asubuhi, gazeti la eDaily rimeripoti.

Wawili hao wameenda jijini Johannesburg, South Africa Jumatano asubuhi kwaaajili ya kushoot video yao mpya na kwajili ya mambo mengine ya kibiashara.Kiba na Baraka

“Ali Kiba na Barakah Da Prince walikuwa pamoja na members wengine wakijiandaa kwa ajili ya mkutano katika moja ya kampuni hiyo katika mji mkuu wa  S.A,” hiyo ni moja ya sentensi iliyoandikwaa na Rockstar4000  kampuni inayowasimamia wasanii hao imesema.

“Wanaume 6,waliokuwa na silaha aina ya bunduki walivamia kwa kuvunja kioo katika office hizo na kuanza kuwashambulia member waliokuwa wanajiandaa kwaajili ya mkutano huo huku wakiwatafuta Ali Kiba NA Barakah Da Prince,” alisikika mmoja wa viongozi wa  Rockstar400.

 
“Kundi hilo liliwavamia Ali kiba na Baraka kwasababu zisizojulikana. Wavamizi hao pia waliondoka na baadhi ya vifaa vya ofisini hapo. Lakini pamoja na yote , Ali Kiba, Barakah Da Prince na wafanyakazi wengine wa kampuni hio pamoja na members wa mkutano huo waliachwa bila majeraha,salama kabisa.

“Ali Kiba na Barakah Da Prince wote wamekumbwa na hofu baada ya tukio hilo. Na wamepewa muda wa siku mbili ili kupumzika na kurudia hali ya kawaida kabla hawaja endelea na mambo mengine. Pamoja na hayo bado wataendelea na project yao ya video ili kukamilisha kilichowapeleka, pamoja na ratiba zao za show zinaendelea kama kawaida nchini S.A. na pande nyingine za dunia zitaendelea kama kawaida,” alimalizia msemaji ahuyo wa ROCKSTAR4000.

Barakah Ameshirikishwa na Ali Kiba katika ngoma yao mpya iitwayo Nisamehe.

Vyanzo vinasema kua Police bado wanachunguza tukio hilo.


Na hii si mara ya kwanza kwa wasanii wa kigeni kuvamiwa nchini South Africa.

Mwaka jana mwisho mwezi wa 12, Msani wa Nigeria Davido, alivamiwa katika duka la  Greyston Shopping Center, Moloko Hotel Junction  muda mfupi tu baada ya kutua nchini humo.

Davido alikuwa pamoja na manager wake, Kamal Ajiboye na mfanyabiashara Chidi Okeke wakati tukio hilo lilipotokea.

Mr Ajiboye alielezea jinsi tukio hilo lilivyotokea katika television ya Za Nigeria

“Tulikuwa ndo tunafika south Africa,tukawa tumesimama katika mataa (traffic light), muda mfupi walikatiza mbele yetu na kusimama wawili wakaja wakiwa na bunduki walizotumia kuvunja kioo cha gari letu”

Wezi hao waliiba pesa,saa za thamani ,mikufu na cheni na passports.

“Walichukua briefcase angu, na mlikuwa na dola USD45, 000, na Davido aliibiwa USD 60, 000. Tulikuwa pia na CEO wa kampuni ya  Mcomm Solution Chidi Okeke ambaye alikuwa na USD80, 000,” Alisema Kamal.

‘’Wote Ali Kiba na Baraka Da Prince wapo sawa na wanapenda kuwahakikishia mashabiki wao kuwa wapo sawa na wanapumzika kwa siku kadhaa kabla ili kusahau tukio hilo la uvamizi kabla hawajaendelea kushoot video yao mpya na kisha kuendelea na project zao barani Africa na Dunia kwa Ujumla.’’ Alimalizia msemaji huyo.
 
 
 
Source:  eDaily Newspaper