
Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga
Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na
Soko jipya zinazoikabiri wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara
mjini Igunga. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana
mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya
basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo
limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu
baadhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na
kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani
ambako nako pia wana sehemu za Biashara.

Rais
Dkt Magufuli akiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John
Mwaipopo wakati akielezea changamoto za Stendi ya Mbasi ya abiria na
Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara
mjini Igunga

Mkuu
wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akiandika maagizo ya Rais Dkt.
Magufuli kuhusiana na Stendi ya Mbasi ya abiria na Soko ambapo ameamuru
huduma hizo zifunguliwe Jumatatu bila kukosa. Rais ameitaka SUMATRA
ihakikishe stendi hiyo inaanza kufanya kazi leo Jumatatu. Pia ameiagiza
halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wafanyabishara waliohodhi sehemu
za biashara bila kuzitumia katika soko jipya wathibitiwe mara moja.

Wananchi
wa Igunga wanalipuka kwa furaha na Mzee huyu anatoa noti ya shilingi
10,000/- akitaka kumtunza Rais Dkt Magufuli kwa kuweza kutatua
changamoto za Stendi ya mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili
wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga

Rais
Dkt Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipokea zawadi ya mchele wa
grade One kutoka uongozi wa wilaya ya Igunga wakati wa mkutano wake wa
hadhara mjini Igunga
Post a Comment