Askofu
wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima inaelezwa kuwa amemjibu
Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kufuatia kauli yake
aliyoitoa Dodoma Julai 23 kuwa Gwajima ni muongo kwa kuwa alisema Rais
Jakaya Kikwete hakuwa akitaka kukabidhi kiti cha uenyekiti kwa Rais
Magufuli kitu ambacho si kweli.
Akihubiri jana kanisani kwake, Askofu
Gwajima alisikika akisema maneno ambayo yalionekana kumlenga Katibu Mkuu
huyo mstaafu, Yusuf Makamba licha ya kuwa hakumtaja jina, alisema kuwa
Leseni yake yeye ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na
maguta.
Siwezi kushughulika na vigari vidogo
vidogo, nyie mnajua leseni yangu ni ya kuendesha semi trailer, alisema
Gwajima wakati wa mahubiri kanisani kwake.
Gwajima amekuwa akikabiliwa na tuhuma za
uchocheza na siku za hivi karibuni alikamatwa uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere na kuhojiwa na polisi kwa maneno yake ya uchochezi aliyoyatoa
kuhusu serikali.
Post a Comment