Mshindi wa BET Awards 2016, kipengele cha Best International Act: Africa ni Black Coffee wa Afrika Kusini.
BlACK COFEE
Ushindi wake umeshangaza wengi. Waliokuwa wanatarajiwa zaidi kushinda
tuzo hiyo ni Diamond na Wizkid. Na kwa mashabiki wengi wa Diamond,
Wizkid ndiye waliyekuwa wakimhofia zaidi. Lakini tulikuja kujipa moyo
kuwa huenda mwaka huu ushindi ni wetu kutokana na msimamo wa Wizkid
dhidi ya tuzo hizo za Wamarekani.
Mwaka jana alieleza sababu ya kutohudhuria akidai kuwa haziwapi
heshima wasanii wa Afrika na UK. Na tangu atajwe kuwania tuzo hizo,
hajawahi kujali, kusema chochote na hakuhudhuria kabisa. Hivyo nafasi
kubwa ilionekana kwenda kwa Chibu. Hata hivyo, BET waliamua kumpa Black
Coffee – Dj ambaye jina lake ni geni kabisa kwa Watanzania wengi.
Black Coffee ni nani?
Jina lake halisi ni Nathi Maphumulo. Ni Dj mwenye mkono mmoja. Alipoteza
mkono wake baada ya taxi kuanguka kwenye kundi la watu ambalo naye
alikuwemo, mtu mmoja alikufa na Black Coffee alikuwa mmoja wa watu 36
waliojeruhiwa.
Ajali hiyo ilimfanya Maphumulo apoteze mkono mmoja ambao umejikunja
kama ngumi na kuwa mfukoni mara nyingi. Mkono wake wa kushoto siku zote
huwa upo mfukoni na bado akiwa na miaka 35, amefanikiwa kuwa na
mafanikio ambayo wengi katika umri huo hawana.
Lakini hakukata tamaa ya kuwa DJ mkubwa ambapo alijiunga na chuo cha
Durban Tech kusomea music production. Kwa sasa Black Coffee ni mmoja wa
majina yanayoheshimika kwenye muziki wa dance nchini Afrika Kusini na
kimataifa pia.
Black Coffee hajawahi kutaka kujulikana kama ‘DJ mwenye mkono mmoja’
kwakuwa anapenda atambulike kwa kipaji chake na sio kwa ulemavu wake.
Alifungua label yake iitwayo Soulistic Music na ameshacheza muziki
katika maeneo mengi yakiwemo Uingereza, Marekani, Ugiriki na kwingine
duniani na huko anaheshimika mno.
Black Coffee kwa sasa anaichukulia hali yake kama baraka iliyokuja na
wajibu kwakuwa kila anachokifanya huwakilisha walemavu. Ana taasisi
yake ya The Black Coffee Foundation ambayo huchangia senti 5 ya kila CD
anayouza.
Mwaka 2010, alipiga muziki kwa saa 60 mfululizo kwaajili ya kuingia
kwenye The Guinness Book of Records kama DJ mwenye mkono mmoja aliyepiga
muziki kwa muda mrefu zaidi ili kuchangia taasisi hiyo.
Miezi miwili iliyopita, Black Coffee alienda Marekani ambapo miongoni
mwa mambo aliyoyafanya ni kualikwa kwenye house party ya Diddy na
kutumbuiza, tena ladha za Afrika.
Diddy alishare kwenye Instagram video ya DJ huyo na kuandika: The
best music at #ultra is HERE!! The World Famous @realblackcoffee
bringing the Africa vibrations live from
#BlueDotUltraWeekend!!#LetsDance #PositiveVibesOnly.”
Naye Black Coffee alirepost video hiyo na kuandika: What a Party!!!!!!what a Legend!!!! Thank you for hosting us @iamdiddy @cassie. Year of the Underdog by @culoedesong #Bless.”
Kama hiyo haitoshi, Coffee alisaini mkataba na label maarufu ya
Marekani, Ultra Records nyumbani kwa wasanii wakubwa wa muziki wa house
wakiwemo David Guetta, Pitbull, Calvin Harris, na Benassi.
Black Coffee akiwa na uongozi wa Ultra Records
Coffee ametoa album yake mpya New Pieces Of Me kupitia label hiyo.
Lakini muhimu ni kwamba tuzo hizi zisitugawe Waafrika. Na hakika
maneno ya Cassper Nyovest aliyekuwa akiwania pia kipengele hicho ni ya
muhimu zaidi.
“African pride!!! Shout out to all the nominees and the winners!!!
Let’s grow with love and God. You’re all beautiful and I love you from
the bottom of my heart!!! My brothers and sisters!!! #Family
#AfricaNa1.”
MakambakoTv.com does not store any files. Everything posted is for promotional use only. Files downloaded should only be kept for 24 hours and then deleted. All music and videos are copyrights to the original owners. Please support the artists and buy their work.
Thank You For Visiting MakambakoTv.Blogspot.com
Post a Comment