[6] [recent] [slider-top-big] [Music]
You are here: Home / Mtoto wa Mabeste kuja na cartoon yake

Mtoto wa Mabeste kuja na cartoon yake

| No comment

Born to be talented. Mtoto wa Mabeste, Kendrick atakuja na cartoon yake itakayoitwa Kendrick Mabeste.

Kendrick ni mmoja kati ya watoto wa mastaa Bongo walioanza kujitengenezea fedha nyingi akiwa na umri mdogo kutoka kwenye dili za matangazo anayoyafanya pamoja na kuwa balozi wa Tabasamu na baadhi ya vitu vingine anavyofanya.

Akiongea na Bongo5, msimamizi wa Kendrick [Lisa Fickenscher] ambaye ni mama yake mzazi, amesema kuwa muda siyo mrefu wataachia cartoon ya Kenderick Mabeste.

“Project za Kendrick zipo on process, ana cartoon ya watoto ya Kiswahili inakuja. Itakuwa ni kama cartoon za kawaida ila itakuwa na muendelezo kama wa tamthilia. Cartoon itakuwa na creativity za kiafrika zaidi,” alisema Lisa.

Aidha aliongeza kuwa cartoon bado wanajipanga kuamua kama watauza CD au itakuwa inaonyeshwa kwenye TV.